Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuikabili Dodoma Jiji leo

B88b406931ffc859c552a0381b1cd100 Simba kuikabili Dodoma Jiji leo

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba leo wanashuka dimbani kuwakabili Dodoma Jiji katika mchezo wa kiporo utakaochezwa kwenye dimba la Jamhuri mjini Dodoma.

Aidha, Namungo leo watakuwa ugenini dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Simba ipo nyuma kwa michezo mitatu ikishika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 35 na Namungo ikiwa nyuma kwa michezo minne dhidi ya wengine ikishika nafasi ya 15 na pointi 18.

Timu hizo zilikuwa zinakabiliwa na michuano ya kimataifa, ambapo Simba ipo Ligi ya Mabingwa Afrika na imetinga hatua ya makundi na Namungo Kombe la Shirikisho ikiingia hatua ya mwisho ya mtoano.

Simba ipo vizuri na inapewa nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo huo kwani katika michezo mitano iliyopita haijapoteza hata mmoja. Klabu hiyo imetoka kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa na bado haijapoteza ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan na suluhu dhidi ya TP Mazembe ya Congo DR katika michuano ya Simba Super Cup iliyomalizika hivi karibuni.

Rekodi hiyo inawabeba wekundu hao wakionekana kuwa hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji inayoongoza kwa kufunga mabao 37 kwenye ligi na kuruhusu matano kwenye nyavu zake hali inayoonesha safu ya ulinzi nayo ipo vizuri.

Simba itacheza mchezo huo ikijua umuhimu wake katika harakati zake za kutetea taji lakini pia ikishinda itakuwa inamkaribia mtani wake wa jadi Yanga iliyopo kileleni kwa pointi 44 ikicheza michezo 18.

Wapinzani wao Dodoma Jiji licha ya kuzidi kushuka nafasi za chini sio timu ya kubeza itapambana kupata ushindi ili kujiondoa katika hatari ya kushuka zaidi. Dodoma Jiji iliyopo nafasi ya 10 haijafanya vizuri katika michezo mitano iliyopita, ikipoteza mitatu na kushinda miwili. Safu yake ya ulinzi haiko vizuri sana ikionekana kuruhusu mabao mengi baada ya kufungwa 14 huku yakufunga yakiwa 12.

Kwa upande wa Namungo, licha ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa inahitaji matokeo mazuri kwenye ligi kwasababu ipo hatarini kusogea nafasi za mwisho. Inacheza na KMC iliyopo nafasi ya saba kwa pointi 22. Mchezo huo utakuwa wa ushindani mkubwa na yoyote ana nafasi ya kushinda kulingana na alivyojiandaa.

Chanzo: habarileo.co.tz