Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kufungwa tena msimu huu! sahau

Simba SC VVV Simba inawakabili Ihefu kesho Novemba 12

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yakiwa yamesalia masaa machache kabla ya mchezo wa Simba na Ihefu pale kwa Mkapa Dar, uongozi wa klabu ya Simba umefunguka kuwa timu hiyo haitafungwa tena msimu huu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahemd Ally alisema, timu ambayo inakuwa inawania ubingwa haiwezi kuwa na matokeo ya kupanda na kushuka, kwa maana ya kufungwa, kushinda na kutoka sare, badala yake inatakiwa iwe inavuna alama tatu tu.

Ahmed alisema, wameshafanya makosa kwenye mechi chache ambazo wamecheza na anatoa kwa ahadi kwa mashabiki wa klabu hiyo kuwa hawataona timu yao ikidondosha alama.

“Najua kuwa inakatisha tamaa kwa timu kama Simba ambayo inagombea ubingwa inakuwa na matokeo ya kupanda na kushuka. Tunatoa ahadi kwa mashabiki wetu kuwa tunakwenda kupambana kwenye kila mchezo.

“Hatutaki kudondosha alama tena kwenye mechi zetu na nawaomba mashabiki waje kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Ihefu kwani uwepo tunahitaji sana,” alisema Ahmed.

Simba wamepoteza mechi na kutoka sare kwenye mechi tatu za ligi hadi sasa, wakiwa wamecheza mechi tisa, wakiwa wamevuna alama 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live