Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kufanya mazoezi usiku kisa Al Ahly

Simba Kufanya Mazoezi Usiku Kisa Al Ahly.jpeg Simba kufanya mazoezi usiku kisa Al Ahly

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamesema wamelazimika kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya siku nane hadi tisa kwa ajili ya kufuata miundombinu sahihi ya kujiandaa dhidi ya Al Ahly.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema wamekwenda Zanzibar kufuata utulivu lakini pia miundombinu ya viwanja inaruhusu kufanya mazoezi muda ule wa usiku ambao utachezwa mechi.

"Mechi yetu na Al Ahly itachezwa saa tatu usiku hivyo tumelazimika kwenda Zanzibar kufaata miundombinu ya kufanya mazoezi usiku lakini pia utulivu kwa mwalimu kuiandaa timu yake kumnyoa Mwarabu Marchi 29," alisema Ahmed.

Simba watavana na Al Ahly katika dimba la Benjamini Mkapa ukiwa ni mchezo wa awali wa Robo ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kurudianiana nao nchini Misri Aprili 5, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live