Klabu ya Simba imetangaza kuanzia Jumatatu, Juni 17 itaanza kutoa taarifa ya wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema watakuwa na awamu tatu tofauti za kutoa taarifa kwa Wanasimba
"Kuanzia Jumatatu tutaanza kutoa taarifa za Thank You, yaani kutoa shukrani kwa wachezaji ambao wameitumikia Simba lakini hawatakuwa sehemu ya kikosi msmu ujao"
"Baada ya zoezi hilo kukamilika, tutaanza kutoa taarifa za wachezaji walioongeza mikataba na tutahitimisha na taarifa za wachezaji wapya tuliowasajili"
"Hiki ni kipindi muhimu sana kwa Wanasimba hivyo tunawaomba wakae karibu na vyanzo rasmi vya taarifa za klabu ya Simba," alisema Ahmed.
TFF tayari imetangaza kufunguliwa kwa dirisha la usajili leo.