Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kabla ya mechi ya Jwaneng hawakuwa vizuri - Nasri

Simba Kabla Ya Meche Ya Jwaneng Hawakuwa Vizuri   Nasri.jpeg Simba kabla ya mechi ya Jwaneng hawakuwa vizuri - Nasri

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka Bongo, Nasri Khalfan amesema hajutii kauli yake aliyowahi kuitoa kuwa Simba haichezi vizuri.

Akizungumzia mchezo uliopita wa Simba dhidi ya Jwaneng, Nasri alisema hiyo ilikuwa mechi pekee ambayo Simba alionesha kiwango kizuri katika mechi za Kimataifa walizocheza ikiwemo na ile ya Wydad.

“Ukiacha mechi Ya Simba aliyocheza na Wydad na Jwaneng, mechi nyengine hakuwa bora, hawakuwa wazuri kwenye ukabaji na ushambuliaji lakini kwenye mechi ya juzi hayo yote wameyafanya kiusahihi,” alisema Nasri.

Nasri alitoa ufafanuzi huu kufuatia kauli alizowahi kutoa kuwa 1. Jwaneng ni bora kuliko Simba 2. Simba sio wazuri kwenye kukaba na kushambulia (haya alisema katika mechi zilizopita Simba alizoonekana ni dhaifu).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live