Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba isikatiwe tamaa inaweza kutoboa

Simba Final Train.jpeg Simba isikatiwe tamaa inaweza kutoboa

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa soka huwa kuna nyakati una matokeo ya kushangaza na ndio maana tunashauriwa tuwe tunaweka akiba ya maneno pale tunapozungumzia mechi fulani.

Unaweza kuipa uhakika mkubwa timu fulani kupata matokeo mazuri na nyingine ukaitabiria kufanya vibaya halafu ndani ya uwanja, mambo yakaenda kinyume ukabaki mdomo wazi.

Na ndio maana nashauri watu wasijisahau na kuamini kuwa Simba imeshaaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupoteza kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza nyumbani.

Maajabu ya soka yanaweza kutokea na Simba ikashangaza kwa kupata matokeo inayohitaji ya kupata ushindi wa kuanzia mabao mawili ili iweze kusonga mbele au hata 1-0 ma ikaimaliza Ahly kwa 'matuta'.

Kuingia katika mchezo huo ikiwa haina cha kupoteza, kutaifanya Simba ijilipue na kucheza soka la kushambulia kwa muda mrefu na kama wapinzani wao watajichanganya na kujilinda basi mnyama anaweza kupindua meza.

Kingine ambacho kinaweza kuipa nguvu Simba ni kiwango kizuri ambacho imeonyesha katika mechi zake mbili zilizopita dhidi ya Al Ahly ambapo ilifanikiwa kutengeneza nafasi ambazo kama ingekuwa makini kuzitumia ingeweza kupata idadi nzuri ya mabao.

Ikumbukwe kwamba sio jambo geni kwa timu kupoteza nyumbani baada ya kupata ushindi ugenini na hata timu kubwa na zenye wachezaji wazuri zimewahi kukutana na matokeo ya kushangaza namna hiyo.

Al Ahly ni timu nzuri lakini haimaanishi kuwa haiwezi kufungwa nyumbani kwani miaka mitatu tu iliyopita iliwahi kuchapwa kulekule Cairo kwa mabao 2-0 na Raja Casablanca.

Simba iende kupambana Cairo, inayo nafasi ya kujitetea na watu hawapaswi kujiaminisha kwa asilimia mia kuwa imeshatolewa.

Chanzo: Mwanaspoti