Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amedai kuwa Klabu ya Simba ndio timu iliyotumia gharama kubwa zaidi kusajili wachezaji wazuri msimu huu kuliko klabu nyingine Afrika Mashariki.
Dauda amesema hayo baada ukikona kikosi cha Simba kwenye mchezo wa Simba Day dhidi ya Power Dynamos wakati Yanga wao walicheza Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
"Yanga SC, imesajili wachezaji wengi sana ila ni wa viwango vya chini sana na bei poa tofauti na Simba SC, ambayo pengine imetumia pesa mara tatu zaidi ya pesa ambazo Yanga wametumia.
"Yanga inaweza kuwa bora ikiwa hawa wachezaji watatokea wachezaji bora na majina kuwa makubwa, ila hadi sasa wako kawaida sana ni 50% kufanya poa wakati huo Simba yenye mastaa kubao pia inaweza kufanya vibaya ila Simba Sc, ni 90% kufanya vizuri kulinga na uwekezaji wao wa pesa nyingi kuliko klabu yeyote Tanzania na Africa Mashariki.
"Na ukinipinga kuhusu usajili wa Simba SC kuwa ndio sajili ya pesa nyingi kuliko klabu yeyote kanda hii wewe huujui mpira," amesema Shaffh Dauda.