Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba imeiacha mbali Yanga - Jemedari Said

Simba X Yanga 1 Simba imeiacha mbali Yanga - Jemedari Said

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said Bin Kazumari amesema kuwa Klabu ya Simba imewaacha mbali wapinzani wao Yanga SC kwenye soka la Kimataifa.

Jemedari amesema hayo kuelekea mchezo wa kesho wa African Football League kati ya Simba na AL Ahly, yakiwa ni mashindano mapya ya CAF huku Simba ikitarajiwa kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza nchini Tanzania kushiriki michuano hiyo.

"Kwani unadhani Yanga walivyoingia fainali Simba walifurahia. Hata wao hawawezi kufurahia Simba kucheza African Football League na kwa kuwa hawana imani kama Al-Ahly anaweza kushinda dhidi ya Simba hawawezi kwenda uwanjani.

"Zamani walikuwa wanaenda kwa sababu walikuwa na uhakika Simba itafungwa. Kama Ahmed Ally anavyosema mwakani hadi IHEFU watashiriki African Football League, aliyeanza kaanza tu.

"Acheni kufichaficha, Simba ndio imefanya Tanzania iogopwe, waarabu zamani walikuwa wakipangwa na timu za Tanzania wanashangilia lakini kwa sasa hawataki kabisa yote Simba ndio kasababisha.

"(Yanga) Wanasema wamewaacha mbali, mbali hiyo wapi, maana inategemea na unatoka wapi. Simba imewaacha mbali sana kimataifa," amesema Jemedari Saidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: