Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba iliwezwa hapa na Prisons

Simbaa+pic Simba iliwezwa hapa na Prisons

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By OLIPA ASSAWACHEZAJI  wa  Tanzania Prisons,  Lambert Sabiyanka (straika) na Salum Kimenya (kiungo), wamefichua siri ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, kwamba imetokana na kujua ubora na mapungufu ya wapinzani wao.

 

Wameliambia Mwanaspoti jana Alhamisi ya oktoba 22, mwaka 2020 mara baada tu ya kumaliza mechi hiyo, iliyopigwa Uwanja wa Nelson Mandela, uliopo mkoani Rukwa, kwamba baada ya kujua mambo hayo mawili, walicheza kwa nidhamu kubwa.

 

Sabiyanka amesema licha ya kuwafunga, Simba sio timu ya kuibeza, amefafanua ina wachezaji makini na kwamba hilo walilijua mapema ndio maana waliamua kuwaheshimu na kujua ni namna gani wanaweza wakapata matokeo mazuri.

 

Chanzo: mwanaspoti.co.tz