Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ilikosea hapa kwa wana lambalamba

Dube Prince Vs Onyango Simba ilikosea hapa kwa wana lambalamba

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imekosa kasi na kupunguza njaa ya kutafuta mabao katika michezo mitatu iliyopita, suala lililochangia kwa kiasi kikubwa kupoteza dhidi ya Azam FC.

Simba ilipoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ilipokuwa wageni wa Azam FC kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, juzi, bao la ufundi la mshambuliaji Prince Dube lilimaliza mechi.

Lakini licha ya kuruhusu bao hilo, Simba ilipiga shuti moja pekee langoni, jambo ambalo linaonekana kuota mizizi, baada ya kupiga mashuti mawili langoni kwenye mchezo wa nyuma dhidi ya Yanga.

Katika michezo mitatu iliyopita ya Simba chini ya kocha Juma Mgunda imefunga mabao mawili, wakati ikiizima Primeiro De Agosto kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, kabla ya sare ya 1-1 na Yanga na juzi kuambulia kipigo mbele ya Azam.

Mgunda alitakiwa kushituka mapema kuanzia mchezo dhidi ya De Agosto, ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 kwa mara ya kwanza tangu kocha huyo wa zamani wa Coastal Union apewe majukumu ya kukaimu ukocha mkuu.

Baada ya mchezo dhidi ya Yanga, Mgunda alisema kulikuwa na makosa katika safu ya ushambuliaji, akiahidi kulifanyia kazi, lakini lilijirudia juzi dhidi ya Azam FC.

“Tulipata tabu ya kupiga langoni, tulicheza na timu nzuri ambayo ilifanya kila njia kutuzuia tusiwadhuru, lakini bado tulitakiwa kufanya zaidi, nadhani ni suala la kurekebisha,” alisema Mgunda baada ya mchezo dhidi ya Yanga.

Shuti pekee katika mchezo huo lililolenga lango lilipigwa na Clatous Chama, ikiwa ni baada ya dakika za kucheza, huku Azam ikionekana kupiga mashuti kadhaa na kupata bao la ushindi.

Kocha Mgunda alisema: “Tulitakiwa kuongeza kasi katika ushambuliaji, hii ndiyo maana tulianza na washambuliaji wawili (Moses Phiri na Habib Kyombo), lakini bado kulikuwa na nafasi hazikutumika ipasavyo.”

Akizungumzia mchezo dhidi ya Azam FC, mmoja wa shabiki wa Simba na mchezaji wa zamani wa Miembeni ya Zanzibar, Erick Semsella alisema anaiona timu hiyo kama iliyoshuka morali katika michezo mitatu iliyopita.

Alisema katika mchezo dhidi ya Azam FC ndipo tatizo hilo lilipokuwa kubwa zaidi, huku akikataa kuwa kukosekana kwa nyota wake wachache kulichangia kipigo chao.

“Simba ilicheza na Yanga, ilipiga mashuti mawili, shukrani ni kwamba moja lilizaa bao, lakini dhidi ya Azam FC iliichukua Simba zaidi ya saa nzima kuhakikisha inapiga golini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live