Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ilifia hapa kwa Raja, Robertinho afunguka

ROBERTINHO KESHO.jpeg Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kipigo walichokipata juzi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco, kimetokana na ubora waliokuwa nao wapinzani wao.

Aidha kocha huyo alisema ubora wa wapinzani wao ulifanya wachezaji wake pia kushindwa kuzitumia nafasi chache walizotengeneza.

Simba juzi ilipoteza mchezo wa pili mfululizo kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni siku chache baada ya kufungwa bao 1-0 na Horoya ugenini Guinea.

Matokeo hayo yameiweka Simba mkiani kwenye kundi D ikiwa haina pointi huku Casablanca wakiwa vinara wa kundi hilo kwa kufikisha pointi sita, Horoya ni ya pili ikiwa na pointi nne na Vipers inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja.

Akizungumza baada ya mchezo huo juzi, Robertinho alisema wapinzani wao walikuwa bora kitu kilichosababisha wachezaji washindwe kutimiza maelekezo ambayo walipeana kabla ya mchezo huo lakini pamoja na kupoteza mchezo huo bado Simba inayo nafasi.

“Hatukuwa kwenye ubora wetu inauma kupoteza mchezo tukiwa nyumbani mbele ya mashabiki wetu lakini tumejifunza kitu naamini tunayo nafasi ya kurekebisha makosa yetu ili kuhakikisha mchezo ujao dhidi ya Vipers tunashinda,” alisema Robertinho.

Alisema pamoja na matokeo hayo kuwaumiza wanapaswa kuyasahau na kuweka nguvu kwenye maandalizi ikiwemo kurekebisha baadhi ya makosa ambayo yamejitokeza kwenye mechi zilizopita.

Alisema haoni sababu ya kumtafuta mchawi kwa matokeo hayo ikiwemo yeye kama Kocha Mkuu kwani amejiunga nayo ikiwa imeshafanya usajili lakini pia hakupata hata nafasi ya kuiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi na mashindano hayo ya kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live