Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba iko vizuri kuliko msimu uliopita - Mrisho Mpoto

Simba Iko Vizuri Kuliko Msimu Uliopita   Mrisho Mpoto.png Simba iko vizuri kuliko msimu uliopita - Mrisho Mpoto

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva na shabiki wa Simba SC, Mrisho Mpoto, amesema safari hii timu wanayo kuliko msimu uliopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mpoto ameshusha ujumbe huu:

Simba ina timu nzuri msimu huu kuliko msimu uliopita na kuliko Klabu yoyote Tanzania.

Tatizo kubwa lililofanya tufungwe ni kusikiliza sauti za nje ya mchezo hasa kwa watu wanaolipwa kwaajili ya kazi hiyo.

Wachezaji walikuwa wanawaza kwamba tukifungwa watu wataongea sana, pia walikuwa wanawaza Kushinda ili watufurahishe mashabiki wao, wakati wanawaza yote hayo timu pinzani wakapata goli la kutangulia mpaka kushinda.

Maoni yangu wachezaji wachezaji wa timu yangu Bora kabisa chezeni mpira wa vipaji vyenu na maelekezo ya walimu tu, acheni sauti za nje mashabiki wapambane nazo zisiwatoe kwenye mchezo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live