Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka East Africa Radio, Ibrah Kasuga amedai kuwa, Klabu ya Simba inapicheza kwenye Uwanja wa Mkapa hasa kwenye michezo ya kimataiwa inakuwa kama Real Madrid ya Hispania.
Kasuga amesema kuwa Simba inao uwezo wa kuujaza uwanja huo kwa full house ya mashabiki 60,000, jambo ambalo huwa linawapa nguvu wachezaji kuona kuwa wanalo deni kubwa la kuwalipa mashabiki zao.
Jumapili ijayo, Machi 3, 2024, Simba atakuwa na ibarua mbele ya Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa katika Uwanja huo wa Mkapa.
"Moja kati ya mechi ambayo Simba walijaza sana uwanja wa Mkapa msimu uliopita ilikuwa ni mechi ya hatua ya makundi dhidi ya Raja Casablanca.
"Ahmed Ally aliita sana watu, Simba walijaa sana kwa Mkapa mpaka kuna shabiki akawa anasema Simba ikicheza kwa Mkapa ni kama Real Madrid, lakini badala yake wakala chuma tatu na wenyewe wakakubali wakasema hii ngoma kweli tumezidiwa kwa sababu ya uwezo.
"Kwahiyo kuna muda unaweza kujaza uwanja lakini bado tutarudi kwenye eneo la ubora, level yako ya ushindani ikoje?, amesema Kasuga"