Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba huenda wakaanza usajili bila Kocha

Mo Dewjiii Simba huenda wakaanza usajili bila Kocha

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakubwa zangu niwaambie kitu? Wazungu wana msemo maarufu wa Eras do come to an end yaani zama huwa zinafika mwisho kama mipango mizuri haitokuwepo, Azam kushika nafasi ya pili sio bahati mbaya, Azam kucheza fainali mbili za FA sio kwa bahati mbaya, maana yake nje ya Yanga tumemkaribisha Mshindani mwingine nae ni Azam.

Kwenye mpira wa miguu kupotea njia ni jambo la kawaida sana, wala sio stori sana Simba kushika UTATU wala kutocheza fainali ya FA zote sio stori, kwangu mimi stori zaidi ni MIPANGO ya kurejea kwenye maeneo yetu, je tuna mipango sahihi? Tupo njia sahihi? Hatuna haja ya presha as long as tuna plans je zipo?

Binafsi naona ni jambo la hatari sana mfano msimu uliyopita Ihefu ana Wachezaji mpaka watano wa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, Azam ana wachezaji hadi nane wa kupata namba kikosi chetu, Yanga ndio usiseme, Coastal Union hakosi wawili maana yake ubora umeanguka mnoo, hili ni dirisha la KUSAJILI haswa.

Azam FC huenda akamaliza usajili wake kabla hata ya mwezi Julai kufika, Yanga huenda akamaliza kuboresha kikosi chake na kusubiri msimu mpya, najaribu kuwaza vipi sie? Ndio kwanza swali la Kocha Mkuu hatuna majibu, anaendelea Mgunda? Ama mnaleta mwingine? Kama mwingine report anapokea lini na kupitia lini ili tuanze kushindana sokoni kupata wachezaji?

Basi Mwenyezi Mungu awatie nguvu Viongozi kwasasa tukomae zaidi na kuiweka sawa timu, tufocus zaidi kwenye timu naamini jua litawaka tena siku moja, the glory days will return.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live