Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba hii ya Kimataifa, wafanya kweli Angola

Simba 3.jpeg Wachezaji wa Simba wakishangilia goli la pili

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wawakilishi wengine kutoka Tanzania wakiahindwa kupata matokeo katika michezo yao, Yanga wakitoa sare nyumbani dhidi ya Al Hilal ya Sudan Ligi ya Mabingwa , huku Azam wakipokea kichapo cha mabao 3-0 ugenini hali ni tofauti kwa mnyama Simba SC.

Simba wakiwa kule nchini Angola wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya wenyeji klabu ya C.D Primeiro De Agosto.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika umepigwa katika Uwanja wa Novemba 11.

Magoli ya Simba waliokuwa katika kiwango bora jioni ya leo yamefungwa na Clatous Chama, Isarel Mwenda na Moses Phiri huku lile la De Agosto likiwekwa kimiani na Dago.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live