Unakumbuka ule wakati wa shida na mateso ambao walipitia Wananchi Yanga ambapo kila msimu walikuwa wanaacha wachezaji zaidi ya 15 na kuendelea?
Unakumbuka ni jinsi gani mashabiki wa Yanga walivyokuwa wanateseka mtaani kwa kutaniwa na mashabiki wa Simba ambao timu yao ilikuwa inafanya vizuri wakati ule?
Sasa ule wakati ndio nauona ukigeuka kwa upande wa Simba baada ya kwenda msimu wa tatu bila ya kutwaa kikombe cha Ligi Kuu na timu yao kupotea hadhi ya nyota 5.
Ili Simba warejee katika hadhi yao lazima wafanye mabadiliko makubwa katika kikosi chao kwa kuacha kundi kubwa la wachezaji na kusajili wengine kama ambavyo iliwatokea Yanga wakati ule.