Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba hatakiwi kudondosha alama leo kama anautaka Ubingwa - Shaffih

Simba Hatakiwi Kudndosha Alama Leo Kama Anautaka Ubingwa   Shafii Simba hatakiwi kudondosha alama leo kama anautaka Ubingwa - Shaffih

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi Shafii Dauda ameshusha uchambuzi wake kama ifuatavyo kupitia ukurasa wake wa Instagram;

Simba V/s Mashujaa ni mchezo ambao Mashujaa wanafikiria kutafuta alama za kuwabakiza kwenye Ligi wakati Simba wenyewe wanafikiria kuendelea kuendelea kuwakimbiza washindani wake wa juu kwenye mbio za ubingwa.

Kwa jinsi vita ya ubingwa ilivyo hadi sasa, Simba haipaswi kuangusha alama yoyote kwa sababu tayari ipo nyuma vinara wa Ligi [Yanga] kwa alama 10 huku wakiwa nyuma kwa alama mbili dhidi ya Azam FC.

Endapo Simba itaendelea kuangusha alama maana yake itakuwa inajiondoa yenyewe kwenye mbio za ubingwa na kuziacha Yanga na Azam kukimbizana.

Baada ya usajili wa dirisha dogo, Mashujaa imeendelea kuimarika siku hadi siku, hawajapoteza mchezo katika mechi sita zilizopita za Ligi Kuu. Hiyo inakupa picha ni kwa jinsi gani timu yao ina mwendo mzuri.

Wakati Simba ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi kwa alama zake 42 baada ya kucheza michezo 18, Mashujaa ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama 21 baada ya kucheza michezo 20.

Kama Simba itashinda mchezo dhidi ya Mashujaa itafikisha alama 45 na kurejea nafasi ya pili huku tofauti ya alama dhidi ya Yanga ikiwa ni saba na timu zote zitakuwa zimecheza michezo 19.

Mashujaa ikipata ushindi itafikisha alama 24 sawa na Kagera Sugar ambayo ipo nafasi ya saba kwenye msimamo, matokeo ya sare yatawaongezea alama moja na kufikisha alama 22 ambazo hazitawasaidia kusogea kwenye msimamo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live