Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba hakuna namna nyingine zaidi ya kushinda mechi ya Jwaneng - Ahemd Ally

Ahmed Ally Awatetea Mastraika Simba .jpeg Simba SC

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikanuni Simba tunahitaji Ushindi mechi ya mwisho ili kwenda Robo Fainali bila kuangalia matokeo ya timu nyingine

KANUNI ZIKO HIVI

Iwapo kutatokea kufungana kwa kitu chochote baina ya Timu mbili na Timu moja wapo inapaswa kusonga mbele mambo yafuatayo yanazingatiwa katika michezo walioyokutana wao wenyewe toka kundi lao:

1. Inaangaliwa Point zao wote wawili 2. Wastani mzuri wa magoli baina yao 3. Magoli mengi ya kufunga ya Ugenini kati yao

SIMBA IKOJE Timu ambazo zinawania nafasi moja na Simba yenye Point 6 ni Jwaneng Point 4 na Wydad Point 3.

Iwapo leo Jwaneng vs Wydad wakatoa Droo itawafanya Jwaneng kufikisha Point 5 na Wydad Point 4 hii itaifanya Simba inabaki nafasi ya Pili na mechi yake ya Mwisho dhidi ya Jwaneng inahitaji Droo ile kusonga Robo Fainali.

Jwaneng Galaxy leo wakishinda watakuwa na Point 7 na kuwa wa Pili kuishusha Simba na kuwaondoa Wydad, Maamuzi yatabaki kwa Mchezo kati ya Simba vs Jwaneng ndio utaamua nani aende kati yao wawili tu

Ikiwa Wydad atashinda leo dhidi ya Jwaneng itafikisha Point 6 sawa na Simba ila haitaiondoa Simba nafasi ya Pili sababu kati ya Timu hizo mbili zilivyokutana mila moja ilishinda nyumbani kwake ila Simba ilishinda kwa idadi kubwa ya magoli hivyo iko juu ya Wydad kivyovyote vile hii inapelekea hata michezo ya Mwisho Timu zote zikishinda Simba ndio itasonga mbele ingawa zote zitakuwa na Point 9 huu ndio utaratibu.

Simba hatuna mbadala mwingine zaidi ya Ushindi dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live