Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba dimbani leo, kuwapima mastaa wake

Mechi Leo Morrocco Kikosi cha Simba SC kikiendelea kujifua

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Simba SC kilichopo nchini Morocco kwa maandalizi ya msimu ujao, Leo Agosti 26 kitashuka dimbani majira ya saa 12 za jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki katika mechi ya kirafiki dhidi ya Olympique club de Khouribga.

Simba ambayo imesajili wachezaji wapya msimu huu inacheza mechi hizo kama sehemu ya kupima maendeleo ya kikosi walichonacho kabla ya ufunguzi wa mechi za Ligi kuu na zile za klabu bingwa.

Hii ni mechi ya pili kwa Mnyama Simba baada ya kuwa ameshacheza mechi ya kwanza dhidi ya FAR Rabbat ya Morocco na kuibuka na sare ya magoli 2-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live