Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba bado tatizo lao liko palepale

Simba Nguvu Moja Simba bado tatizo lao liko palepale

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Yanga jana imeendeleza ubabe dhidi ya Simba msimu huu baada ya kuitandika mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Aziz Ki dakika ya 19' kwa mkwaju wa penalti, bao la pili likifungwa na Joseph Guede dakika 39' akimpiga chenga hadi kipa, Ayoub Lakred.

Mchezo wa mwisho walipokutana katika dabi ya Kariakoo Novemba 05, 2023 Simba SC walifungwa 5-1.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 58 baada ya michezo 22 huku Simba wakisalia na alama 46 kwenye nafasi ya tatu.

Mechi ilikuwaje? Mchezo ulikuwa na risk sana, ukichelewa kidogo tayari upo nje ya move, ndiyo maana utaona ndani ya dakika 15 za kwanza tayari wachezaji wawili(Joyce Lomalisa wa Yanga na Henock Inonga wa Simba) walikuwa wameshatolewa nje kwa tactical sub baada ya kupata majeraha.

Uwanja ulikuwa unateleza sana. Nini kilitokea baada ya kuonekana hivo? Yanga walionesha ubora wao.

Yanga kama kawaida yao 4-2-3-1 , walianza mpira nyuma kwa shape ya 2-3-4-1 (Aucho mbele ya mabeki wawili wa kati, kisha Mudathir anasogea juu kuungana na Maxi, Aziz na Mzize nyuma ya Guede). Yanga waliitaji kuongeza kasi kwenye kushambulia tu.

1: Walipata nafasi kubwa sana nyuma ya kiungo cha Simba, Mudathir, Aziz na Maxi walishambulia vizuri sana kisha ni Yanga tu, kwa sababu walikuwa na runners wengi wakishambulia (Yao, Mzize, Kibabage).

2: Nafikiri kwa zile space walizokuwa wanazipata sambamba Simba hawaweki presha kwenye mpira, ni wao tu, hawakuhitaji pasi nyingi kufika kwenye Defense ya Simba. Simba walikuwa hawaweki presha kwenye mpira na kwa mpinzani.

Simba kwa nafasi walizokuwa wanaziacha aisee, unauliza nini wanafanya kwenye uwanja wa mazoezi hasa wakiwa hawana mpira. Wapo wazi sana, hawaweki presha kwa mpinzani na kwenye mpira. Ngoma, Babacar na Kanouté walikuwa wanapoteza pasi kirahisi sana lakini pia hawakuzuia vizuri.

Simba wametengeneza nafasi tatu ndani ya dakika 10 za mwanzo ambazo zilikuwa clear chances za kupata mabao. Kanoute nafasi 2, Saido, Chama lakini tatizo la umaliziaji liko palepale.

Kibu Denis ni mchezaji mzuri kuwachota mabeki wa timu pinzani lakini tatizo lake naye hajalifanyia kazi, anakimbia sana lakini end product yake inakuwa haina madhara kwa mpinzani.

Nafikiri baada ya kuingia kwa Fred, Luis, Simba waliongeza uhai kwenye eneo la mbele (Movements, idadi ya wachezaji na waliisumbua Defense ya Yanga). Baada ya kuwa 2-1 Yanga waliamua kuzuia kwa kulinda alichonacho.

NOTE:

Yule Aziz Ki “Very Technician” ukimuachia nafasi aisee upo hatarini. Job na Bacca.

Joseph Guedé “ni Striker” amecheza game bora sana.

Chama na Che Malone walicheza vizuri licha ya makosa machache.

Yanga wanashinda Back to Back mbele ya Simba msimu huu.

FT: Yanga 2-1 Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live