Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Simba bado sana"- Mashabiki

Simba Vs Coast Mchezaji wa Simba akijaribu kumtoka Mchezaji wa Coastal Union

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba Sports Club imefanya Usajili wa kiufundi sana msimu huu, kuanzia wale wa kimataifa mpaka wachezaji wazawa.

Tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu huu wekundu hao wa msimbazi wamecheza mechi tatu za kirafiki, mbili nchini Morocco walipokua wameweka kambi na moja dhidi ya wagosi wa ndima, Coastal Union.

Katika mechi zote hizo tatu Simba imetoa sare, mbili za kule Morocco ziliisha 2-2 dhidi ya Far Rabbat, kisha 1-1 na dhidi ya Coastal jana jioni mchezo uliisha kwa sare ya bila kufungana.

Sasa kitendo hicho kimewashtua mashabiki wa Mabingwa hao na kuona pengine bado kikosi hicho hakipo sawa kwani usajili mkubwa umefanyika lakini uwanjani matokeo hayapatikani.

Wakizungumza kwa hisia mashabiki hao wamesema licha ya kuwa kikosi ndio kwanza kinatafutiwa muunganiko lakini angalau dhidi ya Coast Union kungekuwa na matokeo chanya kwa kuwa tayari timu imeshakaa pamoja kwa takriban mwezi sasa.

"Suala la kusema wachezaji wengi wameitwa timu ya Taifa sio sababu, kikosi kina wachezaji wengi maana hata ukisema uwategemee ipo siku wanaweza kuwa majeruhi kwa hiyo kocha atuoneshe basi anawatumieje hawa waliopo kwa kuwa kuna nyakati watahitajika vile vile kutumika" amelalama mmoja wa mashabiki

Chanzo: www.tanzaniaweb.live