Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba bado pointi moja tu kutinga robo fainali

Simba1 Picc Data Simba bado pointi moja tu kutinga robo fainali

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author USHINDI wa 3-0 waliopata Simba dhidi ya Al Merrikh unawafanya Simba kufikisha pointi 10 na kuwafanya wasubiri pointi moja tu ili kujihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali.

Kusubili kwa pointi moja kunatokana na mtu wa pili katika kundi A ambaye ni Al Ahly kuwa na pointi saba huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na AS Vita wenye pointi nne na Merrikh wakiwa na pointi moja.

Kwa maana hiyo zikiwa zimebaki mechi mbili, Simba anahitaji pointi moja tu katika mchezo ujao dhidi ya As Vita na kufikisha pointi 11 akijihakikishia kuongoza kundi A.

Wakati huo Al Ahly wao wakiwa ugenini dhidi ya Al Merrikh hata wakishinda watakuwa na pointi 10 na kuwafanywa washike nafasi ya pili.

Katika mchezo wa Simba dhidi ya Merrikh Kwenye kipindi cha kwanza Simba walionekana kuweza kumiliki mpira huku wakicheza kwa kushambulia wakionyesha kabisa kuhitaji bao la mapema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz