Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba akili yote kumfunga Wydad Jumamosi

KISPIKA CHA AHMED ALLY 1140x640 Simba akili yote kumfunga Wydad Jumamosi

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, kwa sasa nguvu na akili zao zote wamezielekeza kwenye mechi yao ya kwanza ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, mchezo utakaopigwa Jumamosi hii Aprili 23, 2023 katika Dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar.

Akizungumza leo Aprili 19, 2023 kwenye uzinduzi rasmi wa hamasa kuelekea mchezo huo akiwa Chalinze mkoa wa Pwani, Ahmed amesema, ana hakika kama kila mwanasimba ataibeba kauli mbiu yao ya Nguvu Moja na kufika uwanjani kuisapoti timu yao basi hakika watawakanda Wydad.

Amesema kila mwanasimba, akili yake iwe kwenye mchezo huo na anaamini, kwa pamoja wanakwenda kuandika historia ya kumfunga Wydad nyumbani na ugenini ili waweze kufika hatua ya nusu fainali.

"Hakuna jambo lingine lolote tunaweza kuwaza kwa sasa zaidi ya kumfunga Wydad. Kila Mwanasimba anayo nafasi ya kuisaidia Simba kuandika historia ya kuitoa Wydad. Simba ni ya watu, na watu wakiamua jambo lao hakuna linaloshindikana."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live