Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Yatamba Kuongoza Kundi Kimataifa

Simba Dj Simba Yatamba Kuongoza Kundi Kimataifa

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mulamu Nghambi amesema wamepanga kuhakikisha Simba inapata ushindi katika mechi mbili za mwanzo, kwani ndizo zitawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Siku zote mechi mbili za kwanza za makundi ndizo zinaamua kama unaenda robo fainali au hauendi. Hata msimu uliopita, mechi mbili za mwanzo ndizo zilichangia kutufanya tuongoze kundi.

“Kwa maana hiyo tukishinda nyumbani dhidi ya Asec na kisha ugenini dhidi ya Gendarmerie tutakuwa katika nafasi nzuri ukizingatia mechi mbili zitakazofuata zitakuwa dhidi ya Berkane nyumbani na ugenini,” amesema Nghambi.

Ni mara ya kwanza kwa Simba kukutana na RS Berkane na Gendarmerie, lakini imekutana na Asec Mimosas katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2003 ambapo Simba ilishinda bao 1-0 nyumbani na ugenini ikapoteza 4-3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live