Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Yashtukia Janja Ya Asec, Yatangaza Vita

Asec 768x512 1 Simba Yashtukia Janja Ya Asec, Yatangaza Vita

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi hao wamesema qqqwala hawatishiki kwani kichapo kipo palepale.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao utapigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba ipo Kundi D, ikiwa imepangwa pamoja na US Gendarmerie ya Niger na RS Berkane ya nchini Morocco ambayo anaichezea Tuisila Kisinda.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa maandalizi ya kikosi chao yamekamilika, ambacho jana jioni kiliingia kambini sambamba na kuanza mazoezi ya pamoja kuelekea mchezo huo.

Ally alisema kuwa, hadi hivi sasa bado wapinzani wao hawajawapa taarifa za siku za kutua nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo mgumu ambao ni muhimu wapate ushindi nyumbani.

Aliongeza kuwa licha ya wao kutopata taarifa ya siku ya kutua nchini, wanaendelea na maandalizi ya nguvu kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kushinda michezo yote ya nyumbani.

“Sisi kwa upande wetu Simba, tupo katika maandalizi mazuri ya mchezo wetu huu dhidi ya Asec na kikubwa tunazitaka pointi tatu za kila mchezo tutakaoucheza hapa nyumbani.

“Tunafahamu siyo rahisi lakini tutapambana kufanikisha malengo yetu, uzuri timu imeingia kambini leo (jana) sambamba na kuanza mazoezi kabisa.

“Hivyo tumejipanga vema katika hilo, wapinzani wetu hadi kufikia leo (jana) hawajatupa taarifa za ujio wao, hatujui sababu ni ipi,” alisema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live