Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zinatia moyo

Yanga X Simba Moyo Simba, Yanga zinatia moyo

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa zamani wa Simba na Yanga, wameeleza siri ambazo zinaweza kuwabeba vigogo hao kwenye michuano ya Kimataifa.

Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ambaye aliwahi kufanya makubwa na kikosi cha Simba kabla ya kukinoa, alisema ni muhimu wachezaji kuongeza umakini kwenye michezo hiyo kwani kosa moja linaweza kuwagharimu.

“Inawezekana kufanya vizuri hata kama wanacheza ugenini, muhimu ni wachezaji kuwa na nidhamu ya mchezo, naamini wamefanya maandalizi mazuri kilichobaki ni kudhibitisha tu kile walichokifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi,” alisema.

Kwa upande wake, Credo Mwaipopo ambaye aliwahi kuichezea Yanga, alisema,

“Siku hizi mpira wa Tanzania unakua kwa kasi sana, kipindi fulani ilikuwa ni ngumu timu zetu kupata matokeo mazuri ugenini, nadhani ile dhana ya ugenini pagumu taratibu inaondoka.”

Boniface Pawasa mkongwe wa Simba, alisema maingizo mapya kwenye vikosi hivyo yataleta raha wikiendi hii ugenini.

Katika kundi C la Simba kinara ni Raja Casablanca ya Morocco ambayo ina pointi tatu baada ya jana kushinda mabao 5-0 dhidi ya Vipers ya Uganda.

Yanga iliyopo Kundi D ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho itashuka uwanjani kesho dhidi ya monastir.

Chanzo: Mwanaspoti