Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zilivyoweka rekodi kwa Magufuli

A3b306f78025f52858afe7ad4e16acbb Simba, Yanga zilivyoweka rekodi kwa Magufuli

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIGOGO wa soka Tanzania Simba na Yanga ni timu zilizopokezana vijiti kwa kung’ara Ligi Kuu Tanzania Bara na kimataifa katika utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, mwaka huu.

Mwaka 2015 wakati Rais huyo akiingia madarakani, Yanga ilichukua taji la ligi ikitoka kuipokonya ubingwa Azam FC na ikaendelea kutawala hadi msimu wa 2017/2018.

Yanga ilifanya vizuri kipindi hicho ingawa katika michuano ya kimataifa haikuwa katika kiwango kizuri kama ilivyotarajiwa. Watani zao wa jadi Simba ndipo walipoingia kwa kasi msimu wa mwaka 2018/19kwa kuwapokonya majirani zao hao wa Kariakoo (Yanga) baada ya kuchukua taji la ligi mara tatu wakijibu mapigo ya wenzao.

Simba ilikuwa imetoka kupata ukame wa mataji baada ya mara ya mwisho kuchukua mwaka 2012. Ujio wa mwekezaji wao, Mohamed Dewji ulileta faraja na matumaini mapya yaliyodumu hadi leo.

Simba imekuwa ni moja ya timu tishio katika ukanda wa Afrika Mashariki sio tu kufanya vizuri kwenye ligi bali kimataifa baada ya kuwahi kufika robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka juzi.

Pia, msimu huu hadi Magufuli anafariki dunia Machi 17, ameiacha Simba katika kiwango bora hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ikiongoza kundi A kwa kufikisha pointi 10, ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi saba, As Vita pointi nne na Al Merreikh moja na hivyo kuwa kwenye nafasi kubwa ya kufuzu tena robo fainali.

Pia, Yanga ilipata kiwanja Kigamboni walichopewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kimetoka katika utawala wa Magufuli. Timu hizo zinajivunia kila mmoja mafanikio hayo makubwa kwa vipindi tofauti katika uongozi wa kiongozi huyo wa Tanzania.

Chanzo: www.habarileo.co.tz