Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zaweka rekodi ya mabao CAFCL

Simba X Yanga Robo Final Simba, Yanga zaweka rekodi ya mabao CAFCL

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu za Simba na Yanga zimeweka rekodi mbili mpya kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi msimu huu.

Simba ilifuzu hatua hiyo Jumamosi iliyopita, baada ya kuichapa Jwaneng Galaxy mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, huku Yanga ikifanikiwa kufuzu wiki moja nyuma kwa kuifumua CR Belouazdad mabao 4-0, kwenye uwanja huohuo.

Timu hizo zimewekwa rekodi ya kwanza ya kufuzu zote hatua ya robo fainali zikitoka kwenye nchi moja, zikiwa ndiyo pekee kwenye michuano ya msimu huu.

Simba imefuzu ikishika nafasi ya pili kwenye Kundi B kwa kukusanya pointi tisa, huku Yanga ikipitia kundi D, nayo ikiwa nafasi ya pili kwa pointi nane.

Hata hivyo, timu hizo zimeweka rekodi ya kumaliza hatua ya makundi zikiwa zimefunga mabao mengi zaidi kuliko nyingine zote, baada ya kila moja kufunga mabao tisa.

Zinafuatiwa na Belouizdad, Mamelodi Sundowns na Asec Mimosas ambazo kila moja imefunga mabao saba.

Kwenye kipengele cha kuruhusu mabao, Petro Atletic ya Angola ipo kileleni ikiwa haijaruhusu bao lolote, ikifuatiwa na Al Ahly na Mamelodi ambazo kila moja imeruhusu bao moja, Simba na TP Mazembe zinafuata zikiwa zimeruhusu mabao mawili.

Esperance de Tunis, imefungwa matatu, Wydad manne, Yanga na Belouazdad zikiwa kila moja imeruhusu mabao sita.

Timu zilizofungwa mabao mengi zaidi ni Medeama kutoka Kundi D ambalo ipo Yanga mabao 12, sawa na Jwaneng Galaxy kutoka kundi B, ambalo ipo Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: