Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zatamba Ligi ya Wanawake

D97d3f5e64d65a3886cf7039049c711d.jpeg Simba, Yanga zatamba Ligi ya Wanawake

Mon, 30 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu ya Wanwake Tanzania Bara Simba Queens wameanza vyema ligi baada ya kuifunga Mapinduzi Queens kwa mabao 4-2 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Saba Saba, Njombe juzi.

Katika mchezo huo Simba walianza kazi mapema kwani hadi wanakwenda mapumziko walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Wafungaji wa mabao ya Simba ni Opa Clement aliyefunga mawili, Doto Evarist na Mwanahamisi Omar.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Yanga Princess waliifunga Tanzanite kwa mabao 4-0 ambayo yalifungwa na Aisha Masaka aliyefunga mawili, Mwantumu Ramadhan na Amina Ally.

JKT Queens wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo iliifunga Baobab Queens kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Fatuma Mustafa akiandika hat trick ya kwanza kwenye ligi.

Katika Uwanja wa Mashujaa, wenyeji Sisterz ya Kigoma ilikubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Alliance Girls ya Mwanza.

Wageni katika ligi timu ya Es Unyanyembe wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora walikubali kipigo cha mbao 2-0 kutoka kwa TSC Queens ya Mwanza na Ruvuma Queens wakiwa nyumbani Uwanja wa Majimaji Songea walilazimishwa sare ya 1-1 na Mlandizi ya Pwani.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea na mzunguko wa pili Desemba 2 ambapo itachezwa michezo sita pia.

Chanzo: habarileo.co.tz