Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zapishana dakika 5 kwa mkapa

Kiduchu Pic2 Data Simba, Yanga zapishana dakika 5 kwa mkapa

Sat, 25 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KLABU ya Yanga imewasili Uwanja wa Mkapa tumia dakika 5 nyuma ya wenyeji wao Simba kutangulia.

Yanga iliingia saa 9:35 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ikiongozwa na makomandoo waliozungumka eneo la kushukia wachezaji.

Feisal Salum 'Fei Toto ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza kutoka kwenye gari la Yanga wakati wa mwisho akiwa ni kipa Diarra Djigui.

Baada ya hapo benchi la ufundi lilishuka liliongozwa na Kocha mkuu Nasredine Nabi.

Simba na Yanga zimeingia kwa tahadhari Uwanjani hapa huku kila timu ikionekana kutokuwa na amshaamsha kubwa kama tulivyozoea.

Mchezo wa Simba Na Yanga unapigwa saa 11:00, jioni ikiwa ni muda mchache uliosalia kabla ya mtanange huo kuanza.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz