Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zapishana bandarini

Simba, Yanga Waanza Kuweka Viporo Mechi Za NBC Simba, Yanga zapishana bandarini

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa vinara wa Ligi Kuu Zanzibar, JKU SC Salum Ali Haji amesema kwa sasa amehamishia silaha zake Mapinduzi Cup na anataka ushindi dhidi ya Singida Big Stars.

JKU itavaana na Singida leo Ijumaa saa 2:15 usiku, ukiwa ni mchezo wa pili baada ya mechi ya awali kati ya KVZ na Jamhuri saa 10:05 jioni.

Michuano hiyo ambayo ilizinduliwa juzi kwa sherehe kubwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex yataendelea tena leo kwa michezo hiyo mikubwa.

Mapinduzi yamekuwa mashindano yenye heshima kubwa kwa miaka ya hivi karibuni, huku kila mara umaarufu wake ukiongezeka.

WASIKIE MAKOCHA

Salum Ali Haji kocha wa JKU SC, alisema anatarajia mchezo mgumu na wa ushindani kutokana na kucheza na timu ambayo imejaza wachezaji wengi wa kigeni lakini hana hofu kutokana na ubora wa kikosi alichonacho.

“Nawaheshimu Singida Big Stars ni timu ambayo imecheza fainali michuano iliyopita ina kikosi kizuri mchanganyiko wa wazawa na mastaa wa kigeni lakini najivunia vijana wangu walivyo na ubora na vipaji naamini wataendeleza ubora wao huku.

“Nafurahia namna walivyo na ubora na hali ya juu na wamepania kuwa bora kwenye michuano hiyo naamini watapambana kuhakikisha wanatwaa taji la michuano hiyo msimu huu,” alisema.

SBS ambayo msimu uliopita ilifungwa kwenye mchezo wa fainali na Mlandege mabao 2-1, itaanza kibarua hicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu Thank Senong baada ya kumtimua kocha Mbrazili, Recardo Ferreira.

Senong amesema hawana shaka na mashindano hayo na wanaamini kuwa kila kitu kitakwenda vizuri msimu huu.

“Tupo tayari kwa ajili ya kupambania taji msimu huu baada ya msimu uliopita kuishia hatua ya mwisho na kukubali kupoteza kwa mabao 2-1, hatutaki kurudia makosa, tunaamini mchezo utakuwa ngumu lakini hatuna jinsi zaidi ya kupambana zaidi,”€ alisema.

Wakati huohuo, Kocha wa KVZ, Amri Said ‘Stam’ amewatisha Jamhuri ambao watavaana nao mapema leo kwa kuwaambia wanatakiwa kujifua zaidi kuwakabili huku akikiri kuwa wanaenda kuwashushia mvua ya mabao.

“Timu yangu ipo imara kila eneo wachezaji wangu wapo timamu tayari kwa mapambano nafurahia safu yangu ya ushambuliaji kuimarika zaidi huku ukuta wangu nikiwa sina wasiwasi kabisa kwani umefanya vizuri kwenye ligi na moto utaendelea.

“Tutaingia kwa kuwaheshimu wapinzani wetu tumejiandaa vizuri na tunataka kufanya vizuri kwenye mashindano haya ili kujiweka tayari kwa kurudi kupambania taji la ligi,” alisema.

Kwa upande wa Jamhuri wao kama Singida Big Stars timu hiyo ambayo ilikuwa inanolewa na Juma Abdallah Pweka imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba kutokana na sababu binafsi.

Mwanaspoti lilipomtafuta kocha wa timu hiyo alisema hayupo pamoja na timu siku tatu kabla ya ufunguzi wa michuano ya Mapinduzi, hivyo haelewi maandalizi yanaendaje.

“Nimefikia makubaliano na timu kuvunja mkataba siku tatu kabwa ya michuano ya Mapinduzi sijui kinachoendelea kwenye kikosi hicho,” alisema.

SIMBA, YANGA ZAPISHANA BANDARINI

Wakati wakongwe Simba na Yanga wakiwa na mechi za kufuatana Yanga ikitarajiwa kucheza Desemba 31, Mnyama Simba yeye atashuka dimbani Januari Mosi, mmoja anakwenda Zanzibar kesho mwingine keshokutwa tayari kwa michuano hiyo.

Yanga itaondoka Dar kesho, huku Simba ikitarajiwa kuondoka keshokutwa Jumapili na zitamaliza utata kwani ndiyo timu pekee zinazosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka hapa Zanzibar.

Hata hivyo, timu hizo zinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo msimu huu, lakini zinaweza kukutana na hali ngumu kama ilivyotokea msimu uliopita ambao zote zilitolewa kabla ya fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live