Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zapewa waamuzi wa bahati CAF

Waamuzi CAFCL Simba, Yanga zapewa waamuzi wa bahati CAF

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf), limempanga refa Patrice Tanguy Mebiame (30) kutoka Gabon kuchezesha mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Merrikh ya Sudan utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Septemba 30 kuanzia saa 1:00 usiku huku Simba itakayocheza na Power Dynamos uwanjani hapo Oktoba Mosi, ikipewa refa wa Libya, Mutaz Ibrahim.

Mwamuzi Mebiame atakayechezesha mechi ya Yanga amekuwa na neema kwa timu za nyumbani ambazo zimekuwa na historia ya kupata ushindi pindi anaposhika filimbi huku akigeuka shubiri kwa zile ambazo zinakuwa ziko ugenini.

Ni refa anayeonekana sio mnoko sana kwani amechezesha mechi sita za kimataifa ambazo zote zilimalizika kwa timu iliyokuwa nyumbani kupata ushindi na ameonyesha idadi ya kadi 20 tu ikiwa ni wastani wa kadi 3 kwa mchezo, ambapo kadi 19 ni za njano na moja ni nyekundu.

Kwa upande wa Simba, mechi yao dhidi ya Power Dynamos itachezeshwa na refa Mutaz Ibrahim kutoka Libya ambaye ameonekana kutokuwa na uzoefu mkubwa na mechi za kimataifa.

Mwamuzi Ibrahim naye amekuwa na bahati na timu zinazokuwa nyumbani kwani katika mechi 10 zilizopita za mashindano ya Klabu Afrika ambazo amechezesha, timu zilizokuwa nyumbani ziliibuka na ushindi mara tano, sare mbili na wageni walishinda mara moja tu.

Katika mechi hizo, refa huyo ameonekana hana mzaha na wacheza rafu na wachezaji watovu wa nidhamu kwani ameonyesha idadi ya kadi 37, njano zikiwa ni 36 na nyekundu moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: