Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zapewa waamuzi wa bahati

Waamuzi Wa Bahati Simba, Yanga zapewa waamuzi wa bahati

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, Simba na Yanga wamepewa waamuzi wa bahati kwa mwenyeji kwenye michezo yao ya robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo watacheza wikiendi ijayo.

Shirikisho la soka Afrika (CAF), limewatangaza Abongile Tom, raia wa Afrika Kusini, kuwa ndiye atakayechezesha mchezo kati ya Simba na Al Ahly, Ijumaa ya Machi 29 huku Amin Omar wa Misri akichezesha mechi ambayo itachezwa Jumamosi ya Machi 30 kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns.

Waamuzi hao wanaonekana kuwa na bahati kwa wenyeji wa michezo ambayo wamekuwa wakichezesha hivyo huenda Simba na Yanga zikabebwa na hilo.

Katika michezo 10 iliyopita ambayo Abongile amechezesha, wenyeji wameshinda mara saba, ushindi huo ni kwa asilimia 70 huku wakipoteza mara tatu sawa na asilimia 30, mwamuzi huyo ndani ya mechi hizo, amechezesha michuano mitatu tofauti ambayo ni Ligi ya Mabingwa, Kombe la Shirikisho na African Football League.

Ndani ya michezo hiyo, Abongile ametoa kadi 48 na zaidi ya asilimia 60 ya kadi hizo amezitoa kwa timu pinzani.

Aidha, hii itakuwa mara ya tatu kwa mchezo wa Simba kuchezeshwa na mwamuzi huyo, mara ya kwanza ilikuwa Desemba 2023 Mnyama akiwa ugenini (Morocco) alipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca.

Mechi nyingine ilikuwa Oktoba 16, 2022 lakini safari hiyo, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, Abongile aliwahi kuchezesha mechi ya Yanga ambayo Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya Rivers United ya Nigeria kwenye Kombe la Shirikisho.

Kwa upande wa mwamuzi wa mechi ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns, Omar katika mechi 10 zilizopita za kimataifa, mwenyeji ameshinda mara nane ni kwa asilimia 80 huku akipoteza mara mbili kwa asilimia 20 tu.

Kati ya mechi hizo, Mmisri huyo aliwahi kuchezesha mchezo kati ya Simba ikiwa ugenini dhidi ya Horoya, Februari 11, 2023 na Mnyama alipoteza kwa bao 1-0.

Omar ametoa kadi 30 kwenye michezo 10 iliyopita. Waamuzi wote hao sio waumini wa kutoa kadi nyekundu hovyo, msimu huu katika mashindano yote hadi kwenye ligi za ndani kwenye mataifa yao ambazo wamekuwa wakichezesha kila mmoja ametoa nyekundu tatu tu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: