Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zapelekwa Kirumba

Simba, Yanga Warejea Ligi Kuu Jumamosi Simba, Yanga zapelekwa Kirumba

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Shirirkisho la Soka Tanzania (TFF) limeikubalia timu ya Singida Fontain Gate kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kuwa wa nyumbani baada ya uwanja iliokuwa inatumia awali kuufungia.

Kutokana na timu hiyo kuutumia uwanja huo kuanzia sasa, huenda mechi za Singida Fountain Gate za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zikachezwa jijini Mwanza kulingana na ratiba ya michezo husika.

Awali, Singida Fountain Gate ilikuwa inatumia Uwanja wa CCM Liti, lakini imefungiwa kutokana na kutokidhi viwango vinavyohitajika.

Chanzo cha kuaminika kimeiambia Mwanaspoti kuwa viongozi wa timu hiyo walipeleka maombi ya kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kwa mechi zilizobaki - ombi lao limekubaliwa.

"Tutatumia uwanja huo kwa mechi zote za nyumbani. Tunashukuru kwa maombi hayo kukubaliwa," kimesema chanzo chetu.

Mwanaspoti ilimtafuta Ofisa habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza aliyesema kwamba ni kweli ombi lao limekubaliwa na sasa uwanja wa nyumbani ni CCM Kirumba.

"Mapokezi na sapoti ya wadau wa soka jijini Mwanza yanatupa nguvu na tunaamini uwepo wao utatusaidia kuwapa nguvu wachezaji wetu kwenye mechi zilizobaki," amesema Masanza.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: