Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zaonywa usajili 2024-25

Simba, Yanga Zaonywa Usajili 2024 25 Simba, Yanga zaonywa usajili 2024-25

Tue, 11 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amewataka viongozi wa timu za Simba SC, Yanga SC na Azam FC kuwapekeka hospital wachezaji inaowasajili ili kuepuka gharama ya kutibia wachezaji.

Prof. Janabi ambaye yuko katika Kamati ya AFCON 2024 Kitengo cha Tiba amesema kuna umuhimu wa kuwafanyia vipimo wachezaji kabla ya kuwasajili ndani ya timu hizo.

“Klabu hizo ndiyo zina uwezo wa kununua mchezaji hadi Dola Laki Moja, hivyo ni muhimu kabla hawajasaini nao mikataba wawalete tuwapime. Kuna wachezaji wamesajiliwa kwa gharama kubwa na hawajacheza hata mechi moja, sitaki kutaja majina yao," alisema Pr. Janabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live