Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zakwepana robo, nusu fainali FA

Asfc Pic Data Simba, Yanga zakwepana robo, nusu fainali FA

Tue, 11 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SIMBA, Yanga na Azam ambazo zipo nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, kazi kwao baada ya kujua zitakutana na nani Kombe la Azam Shirikisho (ASFC).

Tayari droo imechezeshwa leo Mei 11, 2021 ambapo Simba pekee ndio itacheza nyumbani na Dodoma Jiji, wakati Yanga itaifuata Mwadui FC na Azam itacheza na Rhino Rangers ugenini kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Michuano hiyo ipo hatua ya robo fainali baada ya kupambana tangu hatua ya kwanza ambapo zilikuwa timu 64, 36, 16 na sasa nane.

Simba mtetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam katika droo hizi, imewakilishwa na Khamis Kisiwa ambaye ni meneja wa  mashindano katika klabu hiyo, amesema hautakuwa mchezo rahisi watajiandaa kupambana.

"Dodoma Jiji ni timu yenye ushindani, lakini soka ni kiasi tutakwenda kujiandaa ili kutetea taji hilo," amesema.

Kwa upande wa mwakilishi wa Yanga, Thabiti Kandoro ambaye ni mkurugenzi wa mashindano wa klabu hiyo, amesema amefarijika na uchezeshwaji wa droo hiyo, hivyo wanakwenda kujipanga.

"Kazi imebaki kwetu kwenda kujipanga kuhakikisha tunafikia malengo yetu, ambayo ni kuchukua taji la mashindano hayo,"amesema.

Mechi za robo fainali zinatarajia kuanza kuchezea kati ya Mei 25 mpaka 27.

Mechi za nusu fainali ambazo zitapigwa katika viwanja vya Maji maji Songea mkoani Ruvuma na Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Nusu fainali ya kwanza itazikutanisha msindi wa mechi ya Simba vs Dodoma na Rhino Rangers vs Azam FC huku nusu fainali ya pili itakutanisha mshindi wa mechi ya Biashara United vs Namungo na Mwadui vs Yanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz