Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zagawa dozi U20

Simbayangaa Pic Data Simba, Yanga zagawa dozi U20

Fri, 14 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

DURU ya tisa ya ligi ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20 imeendelea wiki hii kwa michezo tisa kupigwa huku Simba na Yanga wakishinda mechi zao.

Ligi hiyo inashirikisha jumla ya timu za vijana 18 kutoka katika timuĀ  zinazoshiriki Ligi Kuu ambapo inachezwa kwa makundi kukiwa na makundi matatu ya A, B na C huku kila kundi likiwa na timu sita.

Yanga iliyo kundi A iliichapa bao 1-0 Ruvu Shooting ugenini katika uwanja wa Mabatini Pwani huku mechi nyingine za timu hiyo Polisi Tanzania akitoa dozi ya bao 4-1 kwa Namungo, huku Coastal Union na Azam zikitoka sare ya bao 1-1.

Matokeo hayo yanafanya kundi hilo kuongozwa na Yanga yenye alama 15 ikifuatiawa na Azam nao wenye pointi 15 tofauti ikiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika kundi B, Simba walitoa waliendelea kutoa kichapo kwa kuifunga Mbeya City 3-1, ugenini kwenye uwanja wa Sokoine. Mechi nyingine Tanzania Prison ilishinda 4-1 dhidi ya Ihefu huku Mtibwa Sugar wakipokea kichapo cha bao 2-1 toka kwa KMC.

Pamoja na kupoteza mechi dhidi ya KMC, Mtibwa imeendelea kuongoza kundi hilo ikiwa na alama 19 iifuatiwa na Simba yenye pointi 16 wakati Prison wenye pointi 15 wakishika nafasi ya tatu.

Kundi C nalo moto wake sio wakitoto kwani Dodoma Jiji iliitandika Gwambina bao 6-1, Mwadui ikashinda 1-0 mbele ya Biashara United huku Kagera Sugar na JKT Tanzania zikitoa sareĀ  ya 1-1.

Baada ya matokeo hayo Kagera inaendelea kuongoza kundi hilo na pointi 19 ikifuatiwa na Mwadui yene alama 15 huku JKT Tanzania ikishika nafasi ya tatu na alama 13. Ligi hiyo itaendelea wiki hii katika viwanja tofauti.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz