Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zabeba matumaini Kimataifa, Kigogo TFF afunguka

Okwa NElson Simba imesafiri leo kuelekea Angola

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba, Yanga, Azam na Kipanga zikijiandaa kushuka kwenye viwanja tofauti wikiendi hii katika mechi zao za raundi ya kwanza ya michuano ya CAF, kigogo wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Selestine Mwesigwa amezibeba timu hizo kimtindo.

Mwesigwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF enzi za Rais Jamal Malinzi alisema anaziona timu hizo za Tanzania zikipenya kwenda hatua zinazofuata, iwapo zitazichanga karata zao vyema kwenye mechi hizo za awali kabla ya marudiano wiki moja baadaye.

Simba na Azam zitaanza ugenini dhidi ya Primiero do Agosto ya Angola na Al Alkhdar ya Libya, huku Yanga na Kipanga zikianzia nyumbani kwa kuvaana na Al Hilal ya Sudan na Club Africain ya Tunisia kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Mwesigwa alisema anaziona timu hizo zikifanya vizuri kutokana na vikosi zilivyonavyo na hata maandalizi yao, licha ya ugumu wa wapinzani wao hasa kwenye mechi za kuamua timu kwenda hatua inayofuata hasa makundi.

“Tumeshiriki muda mwingi bila kufanya vizuri, lakini Simba imeongeza chachu ya timu zetu kupambana zaidi kimataifa, hivyo naona msimu huu kutakuwa na mabadiliko makubwa,” alisema Mwesigwa aliyewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Yanga.

“Vivyo hivyo kwa Yanga, wana mtu wa kujilinganisha nao, hivyo lazima nao wapambane, Azam imewekeza pia, Kipanga nayo kule Zanzibar haijabaki nyuma, hii inaongeza chachu na mwanya wa timu zetu kujipanga zaidi ili zifanye vizuri,” alisema Mwesigwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live