Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga warejea Ligi Kuu Jumamosi

Simba, Yanga Warejea Ligi Kuu Jumamosi Simba, Yanga warejea Ligi Kuu Jumamosi

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukamilisha majukumu yao ya Kimataifa kwa ushindi mnono, wawakilishi wa nchi katika mashindano ya Klabu Bingwa, Simba SC na Yanga SC, wanarejea kwenye Ligi Kuu ya NBC Jumamosi, Desemba 23, 2023.

Simba ambao walitoka kuwanyoa Wydad Casablanca, wao watakuwa wageni kwa KMC majira ya saa 10:00 jioni huku Yanga waliotoka kuwakaza Medeama watakuwa wageni kwa Tabora United saa 1:00 usiku.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Simba wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 22, Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 25.

Ikumbukwe, Yanga amecheza michezo 10, Simba amecheza tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live