Huyu bwana mdogo kwanza anaitwa Ronwen Hayden Williams kazaliwa 1992 ni kinda mmoja machachali sana.
Mchezo wa juzi yeye ndio Alikua man of the match ukiachilia mbali alivyokuwa anawasiliana na wachezaji wenzie ila anauwezo binafsi.
Kuna penati ya mchongo ilitokea na huyu bwana mdogo aliicheza swafi kabisa kiasi kwamba Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Misri hakuamini na mashabiki vile vile wachezaji wa upinzani hawakuamini kilicho tokea unaambiwa.
Huyu bwana mdogo Tangu hii michuano ianze hakuna mpinzani aliye wahi kumfunga kwa Tafsiri fupi ni kwamba dogo ana cleansheet hadi sasa na ndio Ngoma imeenda Fainali hivyo wanaenda kukutana na Wydad.
Ushauri wangu kwa Sinba na Yanga
Scouting zenu za upande wa Goalkeepers fanyeni kwa umakini maana kunashida pale golini si kwa Simba wala Yanga acheni utoto na mtambue kua mnacheza na Hisia za mashabiki zenu, kama ikimpendeza yeyote kati yenu mchukueni huyu Ronwen Hayden Williams.