Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga waanza kuweka viporo mechi za NBC

Simba, Yanga Waanza Kuweka Viporo Mechi Za NBC Simba, Yanga waanza kuweka viporo mechi za NBC

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpaka sasa tayari vilabu vya Simba SC na Yanga SC zimeshaanza kujiwekea viporo baada ya Ligi kuendelea jana Novemba 22, 2023 na vilabu hivyo vikongwe nchini vikiwa bize kujiandaa na mechi za Kimataifa.

Vilabu hivyo kwa nyakati tofauti vitakuwa vikitupa karata ya kwanza kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo, Yanga atakuwa nchini Algeria hapo kesho kuwavaa CR Belouzdad huku Simba akiwasubiri ASEC Mimosas kesho kutwa Jumapili kwa Mkapa jijini Dar.

Mzungunguko wa kumi wa Ligi ya NBC 2023-24 uliendelea jana na kwa baadhi ya vilabu utaendelea leo na kesho hivyo kuvifanya vilabu hivyo kuwa na kiporo kimojakimoja na usisahau, Simba anacho kingine kimoja alichokipata aliposhiriki Kombe la African Football League.

Mpaka wanacheza mechi zao za pili Kimataifa hatua ya Makundi wiki ijayo Desemba 2, tayari mzunguko wa kumi na moja na wa kumi na mbili utakuwa umeshachezwa hivyo Yanga atakuwa na jumla ya viporo vitatu huku Simba akiwa navyo vinne kwani uwezekano wa kupangiwa mechi hapo katikati ni mdogo.

Kwa mujibu wa ratiba, Desemba 15 na 16 vilabu hivyo viwili vikubwa nchini vitacheza kiporo chao cha mzunguko wa 12. Simba atacheza dhidi ya Kagera Desemba 15 na Yanga dhidi ya Mtibwa Desemba 16.

Hivyo, huwenda kabla ya Desemba 15 na baada baada ya Desemba 16, Bodi ya Ligi itakuwa imeangalia uwezekano wa kumalizia viporo vyao vilivyosalia ambapo Yanga atakuwa navyo viwili huku Simba akiwa na vitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live