Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga waamuzi wale wale

Waamuzi Simba Na Yanga Simba, Yanga waamuzi wale wale

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemtangaza mwamuzi, Issa Sy kutoka Senegal kuchezesha mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Wydad Casablanca utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Rekodi zinaonyesha katika michezo 16 aliyochezesha refa huyo, timu za nyumbani zimeshinda 10, huku zile za ugenini zikishinda minne wakati sare ni miwili na kati ya hiyo ametoa kadi za njano 68 na nyekundu tatu tu.

Mwamuzi huyo amewahi kuichezesha Yanga wakati timu hiyo ilipoifunga Club Africain ya Tunisia bao 1-0 Novemba 9, mwaka jana na kufanikiwa kuiondosha hatua ya mtoano kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa jumla ya 1-0.

Ushindi mkubwa ambao timu ya nyumbani ilishinda wakati Issa akichezesha ni ule wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyoifunga Al Ahly ya Misri mabao 5-2, Machi 11, mwaka huu.

Simba inaanzia nyumbani baada ya kumaliza nafasi ya pili katika kundi 'C' na pointi tisa huku Wydad ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii walimaliza kinara wa kundi lake la 'A' baada ya kukusanya pointi zake 13.

Kwa upande wa Yanga ambao itacheza pia hatua ya robo fainali na Rivers United Jumapili hii kwenye Uwanja wa Godswill Akpabio nchini Nigeria itachezeshwa na mwamuzi, Abongile Tom ambaye anatokea kule Afrika ya Kusini.

Rekodi za Abongile zinaonyesha katika michezo minane ya kimataifa aliyochezesha timu za nyumbani zimeshinda mitano huku za ugenini zikishinda mitatu na kati ya hiyo ametoa kadi za njano 38 wakati nyekundu ni moja tu.

Miongoni mwa michezo aliyochezesha Abongile ni pamoja na ule wa hatua ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba ilishinda bao 1-0 Oktoba 16, mwaka jana na kufuzu hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 4-1.

Chanzo: Mwanaspoti