Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga nani kumkimbia mwenzake Nusu Fainali ASFC

Simba Yanga Robo Simba na Yanga wana nafasi kubwa ya kukutana iwapo watashinda michezo yao ya Robo Fainali

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Droo ya Hatua ya Robo fainali Kombe la Azam Sports Federation imetoka huku Vigogo wa Soka la Tanzania Simba na Yanga wakiwa na nafasi ya kukutana katika hatua ya nusu fainali iwapo tu watashinda michezo yao ya Robo Fainali.

Yanga watakutana na Geita Gold katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam, huku Simba wakikutana na Pamba ya Mwanza katika Uwanja huo huo wa Benjamin Mkapa.

Michezo ya Robo fainali itapigwa kati ya Aprili 8-13.

Michezo mingine ya Robo Fainali ni kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live