Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga na jasho la damu ndani ya Benjamin Mkapa

Yanga, Simba Kukipiga Siku Moja Klabu Bingwa.jpeg Simba, Yanga na jasho la damu ndani ya Benjamin Mkapa

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asubuhi kumekucha, jiji la Dar es Salaam lipo 'busy' na pilika pilika za kila siku, huku mshale wa muda ukiwa unakimbizana na mshale wa sekunde, wengi wakisubiri muda utenganishe asubuhi na mchana iwe jioni ili kuitazama miongoni mwa mechi bora barani Afrika.

Wakati huu kila mtu amebeba imani yake.

Ubora wa mechi ya Kariakoo Derby unabeba kumbukumbu zisizosahaulika. Ipo mechi Yanga waliongoza bao 3, kipindi cha pili Simba alipiga 'comeback' isiyosahulika.

Nani anaweza kulisahau goli la kona la kichuya?

Matukio ya ndani ya uwanja yakizidi kutuachia kumbukumbu zisizoweza kusahaulika kwenye maktaba ya soka, pia nje ya uwanja kuna burudani za mashabiki zinazoweza kukuacha mdomo wazi.

Ni 'mtoko' wa siku si kwa vijana wala wazee, wamama au watoto. Ni mechi inayowaunganisha watu wote.

Ni mechi ambayo haijawahi kuwa nyepesi kwa macho ya nyama, ni mechi ya jasho la damu kwa wachezaji hadi mashabiki.

Mechi inayobeba hisia kali na matukio ya kikatili.

Mara ya mwisho kwenye kariakoo Derby timu moja kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili mfululizo za ligi ilikuwa mwaka 2016, linapokuja suala la kariakoo Derby hakujawahi kuwa na mnyonge hata kama mmoja kati yao ni bora zaidi.

Leo tena tunaenda kuishuhudia moja ya mechi bora ya jasho na damu ndani ya Benjamini Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live