Ngoma ni nzito kwa wawakilishi wa Tanzania, Simba na Yanga kwenye anga la kimataifa kutokana na kilatimu kuwa imara kwenye ushambuliaji huku Simba ikiwa na tatizo kwenye ulinzi.
Roberto Oliveira raia wa Brazil anakiongoza kikosi cha Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku Nasreddine Nabi raia wa Tunisia yupo na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika timu zote zipo hatua ya robo fainali.
Simba kwenye hatua ya makundi ilifunga mabao 10, Clatous Chama raia wa Zambia katupia mabao mannne, Jean Baleke raia wa DR Congo katupia mabao matatu,Sadio Kanoute raia wa Mali katupia mabao mawili Henock Inonga raia wa DR Congo katupia bao moja.
Katika mchezo wa robo fainali ya kwanza Simba ilifunga bao 1-0 Wydad Casablanca mtupiaji akiwa ni Baleke akifikisha bao la nne na Simba kufunga mabao 11 kwenye mechi 7 za kimataifa huku ikiwa imetunguliwa mabao 7.
Yanga kwenye hatua ya makundi ilitupia mabao 9, Fiston Mayele wa DR Congo alitupia mabao matatu, Kennedy Musonda raia wa Zambia alitupia mabao mawili, Jesus Moloko wa DR Congo,Tuisila Kisinda wa Dr Congo, Mudhathir Yahya na Farid Mussa hawa ni wazawa kila mmoja katupia bao mojamoja.
Kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza ubao ulisoma Rivers United 0-2 Yanga mtupiaji akiwa ni Mayele anafikisha mabao matano kimataifa na Yanga inafunga jumla mabao 11 huku ile ya ulinzi ikiwa imefungwa jumla ya mabao manne kwenye mechi 7.