Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba,Yanga kuutangaza utalii Kimataifa

Utalii Pc Dkt Abbas Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Dk Hassan Abass

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Serikali inajadiliana namna bora ya kuzitumia klabu za Simba,Yanga na timu za Taifa katika kuutangaza utalii kupitia mashindano ya Kimataifa.

Pia imesema kupitia filamu ya Royal Tour, imepokea maombi ya timu kadhaa za Ligi ya mpira wa kikapu NBA ya Marekani kushirikiana na Tanzania kutangaza utalii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa, Aprili 28,2023,wakati akitaja mafanikio iliyoipata filamu ya Royal Tour tangu kuzinduliwa mwaka jana,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Dk Hassan Abass amesema tayari Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii na Mkurugenzi wa michezo wamekutana wiki iliyopita kulijadili jambo hilo.

“Mazungumzo hayo ilikuwa ni jinsi ya kuweka mkakati namna bora ya kuzitumia timu za Taifa na klabu kutangaza utalii na mambo yanaenda vizuri"amesema Katibu Mkuu huyo.

Dk Abass amesema kupitia filamu ya Royal Tour, imepokea maombi ya timu kadhaa za Ligi ya mpira wa kikapu NBA ya Marekani kushirikiana na Tanzania kuitangaza Tanzania.

“Kutokana na hamasa ya Royal Tour klabu mbalimbali za Ligi Kubwa Duniani hasa Uingereza, Hispania na Marekani tuko katika mazungumzo nazo, tumeshapokea ofa zao,”amesema Dk Abass.

Chanzo: Mwanaspoti