Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga kupigwa upyaaa

Irudiwe Pic Data Simba, Yanga kupigwa upyaaa

Tue, 11 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa amehitimisha sakata la kuahirishwa kwa mechi ya watani Simba na Yanga na kuafikiana na pande hizo mechi hiyo kurudiwa. Aidha amewaomba viongozi wa klabu na mashabiki kuwa watulivu na kuiamini Serikali kuwa ilikuwa na nia njema na sababu za msingi iliposhauri mechi isogezwe mbele kabla ya kujitokeza mazingira yaliyosababisha Bodi ya Ligi kulazimika kuuahirisha.

Mechi hiyo ya Ligi iliyokuwa ichezwe Mei 8 kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam imeahirishwa na itatangazwa tarehe mpya baada ya kikao kilichofanyika jana usiku.

Katika kikao hicho, kilichohudhuriwa na vigogo wa klabu hizo kongwe na wale wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na bodi ya Ligi, wizara imetoa maagizo manne.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Serikalini, John Mapelele  imesema kufuatia maelekezo yaliyotolewa Bungeni jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, usiku huo huo Waziri Bashungwa alifanya kikao cha mashauriano na pande zote huska.

Kikao hicho kilichowashirikisha viongozi kutoka BMT na wizarani, TFF iliwakilishwa na rais wake, Wallace Karia na Katibu mkuu, Wilfred Kidau, mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto na Mtendaji wake, Almas Kasongo, waziri Bashungwa alifanya mashauriano na pande zote.

Simba iliwakilishwa na mwenyekiti, wa Klabu, Murtaza Mangungu na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Mjumbe wa bodi ya klabu, Zacharia Hanspoppe huku Yanga ikiongozwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, Mjumbe wa Kamati Tendaji, Bahati Mwaseba na Kaimu Katibu Mkuu CPA Haji Mfikirwa. Taarifa ya wizara ilisema makubaliano yamefikiwa mechi hiyo irudiwe, TFF na Bodi wakae haraka iwezekanavyo na kutoa tarehe ya kurudiwa mechi hiyo. "Mashabiki waliokata tiketi waziri ameagiza kituo cha Kitaifa cha Data (Data Center) wanaosimamia mfumo wa N-Card kuwarejeshea tiketi zao kwenye mfumo wa kadi za kuingilia uwanjani mashabiki wote 43, 947, ili tiketi hizo hizo za kielektroniki ziwasaidie kuingia tena uwanjani kwa kila mmoja kukaa eneo lile lile alilokata awali kwenye mchezo wa marudiano,". Pia mfumo wa N-Card uruhusu kuuzwa tiketi zaidi kwa mashabiki wapya watakaoamua kuingia uwanjani siku hiyo hadi kufikia au kukidhi idadi inayoruhusiwa kulingana na uwezowa uwanja Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwepo sintofahamu na kutokuaminiana kati ya baadhi ya klabu hususani Yanga na TFF kuendelea licha ya vikao vya kuiondoa sintofahamu hiyo, hivyo basi waziri ameahidi kuitisha kikao kingine haraka kati ya pande hizo mbili ili kujadili changamoto na kuondoa jakamoyo iliyopo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz