Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga kuongezewa wachezaji wa kigeni, Bodi yafunguka

Kigeni Pic Data Injinia Hersi (Kushoto) akiwa na Aucho

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Almas Kasongo amefafanua taarifa za mabadiliko ya kanuni kwa kuongezeka wachezaji wa kigeni msimu ujao kutoka 10 mpaka 12 akisema kanuni hiyo bado haijapitishwa.

Taarifa ya mabadiliko hayo ya kanuni yalianza kusambaa leo mchana huku bodi ya Ligi wakiwa hawajatoa taarifa yoyote ile hali ambayo ilizidi kuweka sintofahamu kwa wapenzi wa soka nchini.

Kasongo amesema walikaa kikao cha pamoja na viongozi kisha walizungumza baadhi ya mabadiliko ya kikanuni na wanasubiri majibu kutoka kwenye kamati ya utendaji.

"Kanuni zimejadiliwa  lakini bado hazijapitishwa mpaka sasa, kinasubiliwa kikao cha kamati ya utendaji wakae na wao ndio wataweka wazi kwa jamii hivyo tuwe na subira," amesema Kasongo.

Katika mabadiliko hayo ya kikanuni, wachezaji wa kigeni watakaoruhusiwa kucheza mechi kwa pamoja ni saba tu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz