Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga hakuna kulala

9a84cff98fef9acffc3c2cb38fb7a89c Simba, Yanga hakuna kulala

Sat, 14 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VINARA wa Ligi Kuu Simba, Yanga na Azam FC hazitaki kupoteza muda baada ya kujipanga kucheza michezo ya kujiimarisha kwa maandalizi ya ligi.

Azam FC itakuwa katika uwanja wake wa nyumbani kuikaribisha Mbeya Kwanza leo kwa ajili ya kuwapa mazoezi wachezaji wake ambao hawakuitwa kuzitumikia timu zao za taifa.

Kwa sasa ligi imesimama kupisha ratiba ya timu za taifa zinazocheza michezo ya kufuzu fainali za mataifa Afrika,Afcon. Michuano ya Ligi Kuu inatarajiwa kurejea kuanzia Novemba 22, mwaka huu.

Kwa upande wa wanalambalamba hao wa Chamazi msemaji wake Thabit Zakaria alisema Kocha Aristica Cioaba anaendelea kukinoa kikosi hicho na kuwaandaa wachezaji wake kuwa imara na tayari kwa michezo ijayo.

“Tunatarajiwa kucheza mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Mbeya Kwanza, kuwapa nafasi wale ambao walikuwa hawapati namba kikosi cha kwanza lakini pia, ni sehemu ya mazoezi yetu kujiandaa na michezo ijayo.

Kwa upande wa Yanga wanatarajiwa kucheza dhidi ya African Lyon kesho katika uwanja wa Azam Complex ambapo itawatumia wachezaji waliopo na baadhi kutoka kwenye kikosi cha vijana.

Kocha Mkuu Cedric Kaze amekuwa akiendelea na mazoezi kwa wale waliobaki na kuahidi kuwapa nafasi vijana katika mchezo huo muhimu kuwaimarisha kimazoezi.

Mabingwa watetezi Simba wanatarajiwa kucheza keshokutwa dhidi ya African Sports kwenye uwanja huo wa Chamazi.

Simba, tofauti na Yanga na Azam FC wanaojiandaa na Ligi Kuu, mabingwa hao watetezi pia wanajiandaa na Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Katika michezo yao ijayo Azam itakutana na KMC ugenini, Yanga itaikaribisha Namungo na Simba ikiwa dhidi ya Coastal Union.

Chanzo: habarileo.co.tz