Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba , Yanga goma linarudi Kwa Mkapa

Uwanja Wa Benjamin Mkapa Stadium Simba , Yanga goma linarudi Kwa Mkapa

Sat, 3 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Simba na Yanga bado wapo kwenye kizungumkuti cha kutojua timu hizo zitacheza wapi mechi za kimataifa za Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya serikali kutangaza kuufungwa Uwanja wa Benjamin Mkapa sambamba na ule wa Uhuru ambazo timu hizo zilikuwa zikivitumia kama viwanja vyua nyumbani.

Awali kulikuwa na tetesi kwamba huenda mechi hizo zikaenda kupigwa New Amaan Complex, mjini Unguja na kuna walikuwa wakiamini zinaweza kupigwa kwenye viwanja vingine vitakavyokidhi matakwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), lakini sasa taarifa ziwafikie nyote kwamba, goma hilo linarudi tena Kwa Mkapa.

Ndio. Unaweza kusema sasa Simba na Yanga zishindwe zenyewe tu kucheza mechi zao zilizobaki katika makundi ya Ligi y Mabingwa Afrika kwa mechi zilizobakia za nyumbani za Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya serikali kuzilegezea masharti katika matumizi ya uwanja huo ambao mwishoni mwa mwaka jana ulifungiwa ili kufanyiwa marekebisho.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezinasa ni kuwa serikali imeziruhusu Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Mkapa katika mechi za nyumbani za Ligi ya Mabingwa msimu huu, jambo ambalo linazipunguzia presha timu hizo katika kusaka uwanja vipyakwa ajili ya mechi zilizo mbele yao za mashindano hayo kutokanna na mahitaji ya kikanuni.

Ikiwa msimamo wa serikali wa kufungia uwanja huo ungeendelea, Simba na Yanga zingejikuta zikilazimika kutumia Uwanja wa Amaan au kupelekwa nje ya nchi kutokana na viwanja vingine vilivyopo hapa nchini kutokidhi vigezo vya CAF, hjaopo kwenye raundi za awali Yanga iliutumia Uwanja wa Azam Complex, lakini kwa sasa kikanuni zinaukataa.

Yanga iliyosaliwa na mechi ya nyumbani ya Kundi D dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria, awali baada ya Kwa Mkapa kufungiwa, ilikuwa inafikiria kuutumia tena Azam Complex, kwa mechi zilizobakia za kimataifa lakini hilo limeshindikana kwa vile uwanja huo haukidhi vigezo vya CAF.

Kwa mujibu wa muongozo wa ukaguzi wa viwanja wa Caf, viwanja vinavyotumika kwa mechi za kimataifa vimegawanywa katika makundi manne ambayo ni kundi namba moja, namba mbili, namba tatu na namba nne.

Uwanja wa Azam Complex unaangukia katika kundi namba mbili ambalo kikanuni za ukaguzi wa viwanja, hauwezi kutumika kwa mechi za mashindano ya hatua ya makundi na kuendelea katika mashindano ya klabu Afrika.

Tegemeo pekee ambalo lilibakia kwa hapa nchini ni Uwanja wa Amaan Zanzibar ambao Simba hivi karibuni walituma maombi ya kuutumia lakini ibara ya nne ya muongozo wa ukaguzi wa viwanja wa Caf, unaondoa uwezekano wa Simba na Yanga kuwahi kuutumia uwanja huo kwenye mechi zinazofuata kwa vile ombi la kukaguliwa kwake lilipaswa kutumwa angalau miezi miwili kabla ya mchezo husika.

"Nchi mwanachama inaweza kuomba Caf kuendesha kutembelea uwanja na kukagua mipaka yake. Katika mazingira ambayo nchi mwanachama au klabu inatamani kucheza katika uwanja ambao haujathibitishwa na Caf,wanatakiwa waombe Caf kupitia barua rasmi wakiomba ujio wa ukaguzi wa uwanja. Ombi linatakiwa kupelekwa Caf angalau kwa muda usiozidi siku 72 kabla ya mechi ambayo uwanja utatumika," inafafanua ibara hiyo.

Mmoja wa viongozi wa Simba, alilithibitishia Mwanaspoti kuwa, wamejulishwa kwamba watapewa ruhusa ya kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi zilizo mbele yao za kimataifa.

"Nadhani ni jambo ambalo limebakia kutangazwa tu na mamlaka ambayo ni wizara lakini kwa upande wetu tumeshaarifiwa kwamba tutapata fursa ya kuutumia Uwanja katika mechi yetu ya hatua ya makundi dhidi ya Jwaneng Galaxy na iwapo tutafuzu hatua zinazofuata," amesema kiongozi huyo (jina tunalo) na kuongeza;

"Nadhani ni jambo la busara na hekima tu ambalo serikali kupitia wizara imelifanya kwa kuangalia maslahi ya timu zetu ambazo zinawakilisha nchi katika mashindano haya."

Kwa upande wa Yanga mapema Mwanaspoti ilijulishwa kwamba klabu hiyo ilishaandika barua Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutaka ufafanuzi baada ya kufungwa kwa uwanja huo, ilihali walishasaini mkataba wa kuutumia kama uwanja wa nyumbani kwa mechi za kimataifa kulingana na matakwa ya Leseni za Klabu (Club Licence) barua iliyotumwa pia kwa TFF na walishatolewa hofu juu ya mechi za CAF.

"Yanga walishajulishwa kuendelea na maandalizi ya mchezo wao ujao wa CAF, kwani serikali imeshawapa baraka, kama ilivyo kwa mechi zote za timu za taifa na klabu nyingine zinazocheza kimataifa, ila watafute wahusika watawaambia ukweli," kilisema chanzo hicho makini, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo alikiri juu ya jambo hilo.

Gumbo ameliambia Mwanaspoti kwamba ni kweli waliiandikia wizara barua na tayari wameshapewa majibu kwamba waendelee na maandalizi kwani watautumia uwanja huo kwa mechi zote za kimataifa.

"Ilishatujibu kwamba tutaendelea kuutumia uwanja, na kutukata tuendelee na maandalizi yetu ya mechi ijayo ya CR Belouizdad, hivyo tumeshaondoka na presha ya kusaka uwanja mpya," amesema Gumbo.

Yanga itaanza kutupa karata ya mechi ya mwishoni nyumbani Februari 24 dhidi ya CR Belouizdad ambapo ikishinda itajiweka pazuri katika kutinga robo fainali kabla ya kwenda ugenini mwishoni kuvaana na Al Ahly ya Misri Machi 2, siku ambayo Suimba itakuwa inahitimisha mechi ikiwa nyumbani Kwa Mkapa dhidi ya Jwaneng Galaxy baada ya Februari 24 kwenda kucheza na Asec Mimosas ugenini.

Hadi mechi hizo za makundi zikisimama kupisha fainali za Afcon 2023, Simba na Yanga kila moja ilikuwa nafasi ya pili katika makundi waliyopo, Simba ikiwa B na pointi tano, nyuma ya Asec Mimosas yenye 10, huku Yanga ikiwa Kundi D na alama tano pia kama ilizonazo Al Ahly inayoongoza, lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya CR Belouizdad itakayopigwa Februari 16, mjini Algiers, Algeria. Nyota wa zamani wa Simba, Dua Said alisema kama uwanja huo ukifunguliwa, itakuwa faida kwa timu hizo mbili kimataifa.

"Kwanza watafaidika kwa idadi ya mashabiki kuwa kubwa hivyo watapata morali na hamasa kubwa na kingine ni kwamba wakicheza hapo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa itawasaidia wachezaji wacheze vizuri na wawe na hali ya kujiamini kwa kuwa wameuzoea," alisema Dua aliyewahi kuwika pia Small Simba ya Zanzibar na Mtibwa Sugar.

Chanzo: Mwanaspoti